Wabunge waipongeza Wizara ya Maliasili
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania wameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa Kazi nzuri inayoifanya ya kuhifadhi raslimali kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye huku wakisisitiza ushirikishwaji wa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.