Utata vifo vya vichanga, mmoja akutwa amechunwa
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linaendelea na uchunguzi kufuatia utata wa vifo vya watoto mapacha ambao walizaliwa njiti katika kituo cha afya Kaliua kilichopo mkoani humo ambapo mtoto mmoja alikutwa ameondolewa ngozi ya paji la uso na kuharibiwa jicho moja la upande wa kulia.