Daktari feki akamatwa Njombe akitoa huduma za afya
Kijana mmoja aitwaye Ahmed Abdallah mkazi wa kijiji cha Mapogolo kata ya Milo wilayani Ludewa mkoani Njombe, amekamatwa na polisi baada ya kugundulika kutoa huduma ya afya kwa miaka 18, kinyume cha sheria ikiwemo mazingira yasiyo salama na kutokuwa na vyeti vya taaluma hiyo.