Bunge laidhinisha bilioni 295.9 Wizara ya Mifugo
Bunge limeidhinisha bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yenye thamani ya shilingi bilioni 295.9, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 112 kitatumika kwenye sekta ya mifugo huku shilingi bilioni 183 zikienda kutumika kwenye sekta ya uvuvi.