"Jeshi la uhifadhi linafanya kazi vizuri"- Masanja
Serikali imesema taasisi za uhifadhi nchini zimeendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo kufuatia muundo wa sasa wa Jeshi la Uhifadhi kuziwezesha taasisi hizo kufanya kazi zake vizuri huku kila taasisi ikiwa inasimamiwa na Kamishna wa Uhifadhi.