"Real Madrid ni Real Madrid" - Ronaldo
Cristiano Ronaldo amesema Real Madrid, walistahili kuifunga Bayern Munich, kwa kuwa walicheza vizuri, na yeye mwenyewe kafurahia, kufunga hat-trick, katika ushindi wa mabao 4-2, mchezo wa marudiano hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Barani Ulaya.