Serengeti watumia dakika 5 kuweka heshima
Dakika 5 kati ya 10 za nyongeza zimetosha kuipa sare ya mabao 2-2 timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys dhidi ya vijana wenzao kutoka Ghana, Black Starlets katika dimba la Taifa Dar es Salaam.