Alichokisema Nay wa Mitego kuhusu Vanessa Mdee
Msanii wa bongo fleva Nay wa Mitego amemtaka msanii mwenzake Vanessa Mdee kuwa jasiri katika kipindi kigumu anachopitia cha kushikiliwa na polisi na kumtia moyo kwamba aone mambo hayo yanayomkabili ni changamoto za kufikia mafanikio.