Wanawake watakiwa kutoogopa ushindani wa kisiasa
Wanawake wametakiwa kujiongezea elimu na kushiriki katika vinyang’anyiro vya kugombea nafasi mbalimbali za maamuzi na uongozi ili waweze kupigania haki zao wakiwa viongozi wenye weledi badala ya kuacha wanaume kushika nyadhifa zote za maamuzi.