
Felix Lyaniva
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya Temeke Mheshimiwa Felix Lyaniva alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Wilayani Temeke.
Lyaniva amesema miongoni mwa changamoto katika kupigania haki za wanawake na kuepuka ukatili wa kijinsia ni wanawake kujiweka nyuma katika kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanawake wasiokuwa na elimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto James Kibamba alipomwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema wizara iliamua kuanzisha mfuko wa wanawake ili kuwawezesha wanawake kupata mitaji ya kuendesha biashara zao
Amebainisha kuwa mpango huo wenye lengo la kutoa mikopo kwa wanawake utaendelea kwa halmashauri zote nchini.