Posho ya mbunge yatumika kujenga zahanati 8
Posho ya vikao ya mbunge wa Singida Magharibi Mh. Elibariki Kingu, imetumika kuanzisha ujenzi wa zahanati nane katika jimbo hilo, ikiwa ni njia ya kutekeleza uamuzi wake wa kutochukua posho hizo, na badala yake akitaka ziwatumikie wananchi.