Judo watakiwa kuthibitisha ushiriki ligi ya taifa
Vilabu shiriki vya michuano ya Klabu Bingwa Taifa ya mchezo wa Judo vimetakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Novemba 12 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa uongozi kupanga ratiba ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Novemba 19 mwaka huu DSM.