Mauzo Soko la Hisa la Dar es Salaam yaongezeka
Idadi ya mauzo katika soko la hisa la Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 39 kutoka shilingi bilioni 3.8 na kufikia shilingi bilioni 5.3 kwa mujibu wa taarifa za mwenendo wa biashara katika soko hilo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.