Mapigano Congo yapelekea vikwazo dhidi ya Rwanda
Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Ulaya (EU) zimeelezea kushtushwa na hali inayoendelea kuzorota katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasia ya Congo, na kutoa onyo dhidi ya hali ya mgogoro na ukiukaji wa uhuru wa kisheria wa nchi hiyo.