TAMWA wasikitishwa na unyanyasaji wa mtandaoni
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeiomba serikali kuhakikisha sheria ya mtandao inasimamiwa kikamilifu na kwa wakati wote kwani vitendo vya uhalifu wa mtandao bado vinaonekana kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii.