Mashali kuwaongoza mabondia wa Tanzania kusaka UBO
Bondia Mtanzania Thomas Mashali ametamka wazi kuwa leo Mei 14 itakuwa siku ya kukumbukwa na Watanzania hasa wapenda michezo wa masumbwi, pale atakaoipeperusha vema bendera ya taifa akimpa kipigo kizito bondia Sajjad Mehrab wa Iran kesho.