Saratani inadhoofisha nguvu kazi ya taifa
Ugonjwa wa Saratani umetajwa kuwa kikwazo cha uzalishaji mali nchini kutokana na ugonjwa huo kushambulia zaidi vijana wenye umri wa miaka 25 hadi 45 ambao ndio nguvu kazi ya taifa hivyo jamii imetakiwa kujenga tabia ya kupima kama wana ugonjwa huo.