Baraza la Madiwani lamkataa afisa elimu
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera, limemkataa Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo, Hellen Lugumila, kwa tuhuma za uzembe na kusababisha wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya shule za sekondari kimkoa.