Watanzania wachache wanaotumia huduma za kibenki.
Idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kifedha zinazotolewa na mabenki nchini imekuwa hairidhishi ambapo katika kutambua hilo Amana Benki yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeamua kutoa zawadi kwa Watanzania watakaoweka fedha zao katika benki hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo pasipo kuzichukua.