Kipindupindu chazidi kuteketea Tanzania
Maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini yameendelea kupungua ambapo takwimu za mwezi wa Aprili 2016 zinaonesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 1,037, sawa na punguzo la asilimia 65 kutoka wagonjwa 2,953 walioripotiwa mwezi Machi 2016.