Kuna mpango wa kutupunguza makali-Mwika
Kamati ya nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana kupitia kesi za washambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, huku wazee wa klabu hiyo wakisema hawatakubali endapo wachezaji wao watafungiwa. Baraza la Wazee wa klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani jijini Dar es salaam limesema limeshtukia hujuma zilizopangwa kuwavurugia mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu. “Kuna taarifa za chinichini kuwa kamati ya nidhamu imepanga kuwafungia Ngoma na Tambwe, hizi ni njama za kutupunguza makali alisema Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Hashimu Mwika".