Hazina: UDA inamilikiwa na Simon Group kwa 51%
Ofisi ya Msajili wa Hazina imesema serikali ya Tanzania haijauza asilimia 49 ya hisa zake kwa kampuni ya simon Group ili kuendesha mradi wa mabasi ya UDA na badala yake halmashauri ya jiji la Dar es salaam ndio imeuza asilimia 51 ya hisa zake kwa kampuni hiyo ambayo hivi sasa inamiliki hisa hizo baada ya kumaliza malipo ya hisa zilizobaki mapema mwezi huu.