Mkoa wa Songwe sasa kutambulika rasmi
Ofisi ya sasa ya mkuu wa wilaya ya Mbozi ambayo pia ilikuwa inatumiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo imeteuliwa kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe hadi pale serikali itakapokamilisha ujenzi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa huo.