Yanga SC dhidi ya Mashujaa kesho KMC Complex

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Namungo FC ikipoteza dhidi ya Azam FC, Tabora United,Al Hilal,MC Algers na kutoka sare dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa makundi wa ligi ya mabingwa Afrika.

Yanga SC itashuka uwanjani kesho kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya timu ya Mashujaa kutoka Kigoma kesho saa 10:00 jioni uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS