Tanzania yashika nafasi ya Tatu Ndondi Afrika

Mchezo wa ndondi unakua kwa haraka nchini Tanzania pamoja na kuongeza Mashabiki wapya kutokana na nguvu kubwa inayotumika kuutangaza mchezo huo.Mafaniko ya Bondia Hassan Mwakinyo yamewafanya Vijana wengi kuuona mchezo wa ndoni kama sehemu ya kuweza kubadili maisha yao na ya Familia zao.

Tanzania inashika nafasi ya tatu katika nchi zinazofanya vizuri kwenye ubora wa ngumi za kulipwa barani Afrika kwa mujibu wa taarifa ya viwango vilivyotolewa January 2025 na  shirikisho la mkanda wa ABU.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS