Mafuriko yaleta majanga Afrika Kusini
Afrika Kusini imetangaza mafuriko yaliyotokea nchini humo kuwa janga la kitaifa baada ya mvua kubwa kusababisha majimbo yake saba kati ya tisa kufurika, kuharibu barabara na madaraja na kuwaacha wakulima wakipata hasara.

