UNHCR yajenga makazi kusaidia wakimbizi DRC
Takriban nyumba 3,000 zimejengwa Bushagara, kaskazini mwa mji wa Goma nchini DRC Congo ili kuwapokea wakimbizi wa ndani wanaoishi katika hali ngumu kutokana na kukimbia mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa M23.