Serikali yahamasisha michezo kwa watoto
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amesema kuwa, miongoni mwa mipango ya Serikali katika kuziendeleza timu za Watoto ni pamoja na kuendelea kuratibu mashindano ya michezo ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISSETA).