Kijana ajiua kisa pesa ya soda
Bukindu Mhoja (22), mkazi wa Kitongoji cha Bugogo, Kata ya Bukoli mkoani Geita amejiua kwa kunywa sumu, baada ya kudaiwa hajalipa shilingi 45,000 ya soda alizokuwa ameagizwa kwenye duka la Masikio ambaye alimpokonya vinywaji na kumsema kwa maneno mabaya.