Rais Samia ana mapenzi na sekta ya mifugo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Siku Mbili wa Wadau wa Sekta ya Mifugo kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma, Disemba 19, 2022. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angela Kairuki na wa tatu kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana mapenzi ya dhati na Sekta ya Mifugo na anatamani kuona inaleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kukuza zaidi pato la wananchi, kutoa ajira na kuchangia pato la Taifa bila kuathiri mazingira na maendeleo ya sekta nyingine