Mwili wa Brigita wapatikana umeharibika
Mwili wa Brigita Sanga (Pude) ambaye alikuwa ni ndugu wa marehemu Neema umepatikana ukiwa tayari umeharibika ikiwa ni takribani wiki moja tangu yatokee maafa ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne na kufukia watu katika eneo la Kariakoo Dar es Salaam tukio lililopelekea vifo na majeruhi.