Korea kuipa Tanzania mkopo wa kulipa kwa miaka 40
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 zitakazotolewa kwa njia ya mkopo nafuu kwa Tanzania kupitia Mfuko wa Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF), kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.