Lee Carsley amaliza muda wake England

Carsley alichukuwa nafasi ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Gareth Southgate aliyejiuzulu baada ya michuano ya UEFA Euro 2024. Ameiongoza timu hiyo michezo sita akifanikiwa kushinda michezo mitano na kupoteza mmoja dhidi ya Ugiriki uliofanyika mwezi Oktoba 2024.

Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Lee Carsley amemaliza muda wake wa kufundisha timu ya taifa hilo kwenye mchezo dhidi ya  Ireland ambao umetamatika kwa kikosi cha Simba watatu kushinda kwa ushindi mnono wa goli 5-0 ushindi huo umeifanya England kufuzu kucheza Ligi A.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS