Polisi Kagera waua mmoja anayedhaniwa ni jambazi
Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi na askari polisi, wakati yeye na wenzake wawili wakijiandaa kufanya uhalifu katika kituo cha mafuta cha Benaco Oil, katika kijiji cha Rwakalemera kata ya Kasuro tarafa Nyamiaga wilaya ya Ngara, mkoa wa Kagera.