Sead Ramovic kutangazwa Yanga SC kuwa Kocha mpya

Nyota huyo wa zamani wa VfL Wolfsburg na Borussia Mönchengladbach anatarajiwa kufanya makubwa kikosi cha Yanga FC kutokana na kurithi kikosi chenya Wachezaji bora walio washindani.Kazi yake ya kwanza itakuwa kurudisha viwango vya Wachezaji vilivyoporomoka, pili kusimamia nidhamu za Wachezaji wa kikosi hiko kutokana na kuvuja kwa taarifa kuhusiana na nyota wengi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kuendekeza starehe na kuporomosha viwango vyao.
Sead Ramovic anaweza kutangazwa muda wowote kuanzia sasa klabu ya Yanga SC kuwa Kocha mpya wa timu hiyo baada ya kumfukuza kazi aliyekuwa Kocha wake Miguel Gamondi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo klabu kwenye ligi kuu Tanzani bara.