Yanga SC yaachana na Kocha wake Miguel Gamondi

Miguel Gamondi alijiunga na Yanga SC Juni 2023 kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwalimu wa timu hiyo ya Wananchi Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye alitimkia AS FAR Rabat ya nchini Morocco.Gamondi anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kufundisha mpira wa kushambulia na burudani kutokana na asili yake ya America ya Kusini kucheza mpira huku ukiwa na tabasamu mdomoni mwako.Ameiongoza timu ya Wanajangwani kushinda Kombe la Shirikisho Tanzania, Kombe la Ligi kuu Tanzania bara pamoja na kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Klabu ya Yanga imetangaza kuachana na Kocha wake Miguel Gamondi hii leo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na timu hiyo kupitia ukurasa rasmi wa Instagram klabu hiyo.Klabu hiyo pia imesitisha mkataba wa aliyekuwa msaidizi wa Muargentina huyo Moussa Ndaw.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS