Wananchi Kondoa walipwa milioni 40
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imelipa kiasi cha shilingi milioni 40 ikiwa ni kifuta jasho/machozi kwa wananchi 198 wa Vijiji vya Chemchem, Tungufu, Tampori, Mulua na Iyoli wilayani Kondoa kutokana na kupata madhara yaliyosababishwa na wanyamapori.

