"Taarifa ya ajali ya ndege bado haijatoka" -Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kwamba serikali bado haijatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Presicion Air iliyotokea Novemba 6, 2022, hivyo taarifa inayosambaa mitandaoni ipuuzwe kwani haijatolewa na mamlaka rasmi za serikali.