Wenye Kifua Kikuu wasinyanyapaliwe - Wanaharakati
Watanzania wametakiwa kutowanyanyapaa watu wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu kwani kitendo hicho hakiwezi kumaliza maambukizi ya ugonjwa huo na badala yake wawashauri na kuwaonesha mahali wanapoweza kupata tiba sahihi ya ugonjwa huo.