Wambura wa Coastal Union mchezaji bora wa Februari
Kiungo wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari mwaka huu wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.