Uongozi Yanga SC unapswa kuwa na uvumilivu

Timu zinapopitia wakati mgumu huwa vitu vingi huwa vinabadilika maswali yanakuwa mengi kuanzia kwenye ubora wa benchi la ufundi mpaka namna Wachezaji wanavyojituma kwenye michezo wanayocheza. Kuna kipindi timu huwa zinapitia wakati mgumu kwa fomu yake kushuka Wachezaji wote wanakuwa wapo chini kiuchezaji inahitaji uwezo mkubwa wa Mwalimu kuweza kurudisha hali ya upambanaji kwenye kikosi chake kwa kuhakikisha ari kwa Mchezaji mmojammoja ili timu irejee kwenye hali ya kawaida.
Klabu ya Yanga inapitia kipindi kigumu kwasasa kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata siku za karibuni.Imepoteza michezo mitatu mfululizo kitu ambacho hakijazoeleka na Mashabiki pamoja na Wanachama wa timu hiyo.