Mke wa Mutta akiri kuchoka, adai hamtafuti tena
Mke wa diwani wa Kawe jijini Dar es Salaam Mutta Rwakatare, amekiri kutokujua ni wapi alipo mume wake huyo kwani hadi sasa unakaribia mwezi wa tatu bila diwani huyo kuonekana nyumbani na kusema amechoka na tabia hizo na hatohangaika tena kumtafuta.