Uhusiano Tanzania na Rwanda sio mzuri - Membe
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Bernard Membe, ameweka wazi na kufafanua kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda bado sio mzuri na kwamba juhudi za kurejesha katika hali yake ya kawaida zinaendelea.