Ambaka msichana aliyepooza mwili
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Musoma, imemhukumu miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 3 Juma Ligamba (52) mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara, baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji kwa binti wa miaka 19 ambaye amepooza viungo vyake.