"Hatuko kwenye uchumi wa kati" - Prof Muhongo
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo, amesema kwamba nchi ya Tanzania haipo tena kwenye uchumi wa kati, kwani imeshuka na kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu pato la mtu mmoja mmoja litafikia dola za kimarekani 990.