TFF yafuta kiingilio Stars VS Sudan kwa Mkapa

Mchezo wa marudiano wa kufuzu kushiriki michuano ya CHAN 2025 kati ya timu ya taifa Taifa Stars dhidi ya Sudan uliopangwa kuchezwa uwanja wa Benjamini Mkapa hautokuwa na kiingilio ili kuwezesha Watanzania wengi kuingia uwanjani kuishanglia timu ya taifa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugegeni nchini Mauritania kwa kufungwa goli 1-0.

Taifa Stars imeshafuzu michuano hiyo kupitia tiketi ya Uenyeji wa mashindano hivyo inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kurejesha imani kwa Watanzania kwenye timu ya taifa baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Congo DRC,  kufuzu michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS