Wazazi Waonywa kuwafungia Watoto Maalbino
Wazazi nchini wameombwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu wa ngozi albino na badala yake wawapeleke shule pale wanapofikia umri wa kuanza shule ya awali.
Katibu wa Chama cha maalbino wilaya ya Temeke Bw. Gaston Mcheka amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafungia ndani watoto walemavu wa ngozi kwa kuona kuwa ni nuksi na mkosi katika familia zao.