Msichana atuhumiwa kwa uchawi, akutwa na mchanga
Flora Juma (18), ambaye amekuwa akifanya kazi za ndani katika familia moja iliyopo mtaa wa Kombo Masai, Kata ya Malolo Mjini Tabora, amejikuta yuko matatani kwa kutuhumiwa na uchawi, baada ya bosi wake kukagua na kukuta begi lake lina dawa za kienyeji.