Jumatano , 26th Oct , 2022

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Bw. Rishi Sunak ameteua timu yake ya mawaziri katika siku yake ya kwanza kama waziri mkuu wa Uingereza.

Bw. Rishi Sunak Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Katika hotuba yake muhimu nje ya makao makuu ya Waziri mkuu amsema anataka kuleta nchi na chama pamoja, akiahidi utulivu wa kiuchumi na amani.

Mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliona chaguzi zinazoweza kutabirika, na zingine ambazo zimewashangaza wabunge, huku kipengele kingine muhimu cha mabadiliko haya kikiwa ni utulivu katika nafasi tatu za juu: Jeremy Hunt kama kansela, James Cleverly kama katibu wa mambo ya nje na Ben Wallace kama waziri wa ulinzi.

Mojawapo ya teuzi zinazovutia sana ni kurudi kwa Suella Braverman kama katibu wa masuala ya ndani. Braverman alijiuzulu siku chache zilizopita baada ya kukiuka taratibu za usalama, alipotuma hati ya serikali kwa mtu ambaye hajaidhinishwa kuipokea.

Bw Sunak pia amewarudisha wafuasi wengine wakuu kwenye majukumu ya juu - kama Dominic Raab, Steve Barclay na Oliver Dowden ambao hatahivyo, walikuwa watu muhimu katika kampeni yake wakati wote wa kiangazi, walituzwa kwa uaminifu wao na majukumu serikalini.