LeBron James na Mtoto Wake waweka historia NBA

Mfungaji bora wa muda wote wa NBA LeBron James usku wa jana Oktoba 22, 2024 aliweka rekodi nyingine kwenye ligi ya kikapu Marekani maarufu NBA. King aliweka rekodi ya kuchangia uwanja na mwanawe LeBron ‘Bronny’ James Jr mwenye umri wa miaka 20 kwenye mchezo uliozikutanisha LA Lakers dhidi ya Minnesota TimberWolves waliposhinda vikapu 110 kwa vikapu 103.
Familia ya Lebron James imefikia rekodi iliyowekwa na Familia ya Ken Griffey aliyecheza na Mtoto wake Ken Grifey JR uwanja mmoja kwenye timu ya Seattle Mariners michezo ya ligi ya kikapu Marekani msimu wa 1990-1991, walicheza kwa pamoja michezo 51.